Hero image

Coca-Cola x FIFA World Cup 2026

Hisi Yote Challenge

Rekodi Video  |  Post  |  Shinda Zawadi

Mpira si wa kutazama tu. Ni hisia. Tuonyeshe hisia zote. Iwe ni furaha, huzuni, utani na matumaini yako – Na ujipe nafasi ya kushinda zawadi.

June 20 -- July 25, 2026

Jiandikishe Sasa Angalia Nafasi Yako

Jinsi ya Kushiriki

1

Jiandikishe

Jaza fomu ya usajili.

2

Buni

Rekodi video ukitazama mechi yoyote msimu huu wa Kombe La Dunia La FIFA 2026 huku ukiburudika na Coca-Cola.

3

Chapisha

Shiriki kwenye TikTok na/au Instagram. Tagi @coca_cola_tanzania, #NiWakatiwaCocaCola, na #NiMsimuwaFifaWorldCup.

4

Shinda

Washindi wa tatu bora kila wiki watapata zawadi.

Fomu ya Usajili

Zawadi za Pesa

Pata Pesa Kulingana na Views Zako

Views zako zinahesabiwa kwa jumla katika wiki 6 zote za changamoto, kwa kuchanganya Instagram na TikTok. Kadri video zako zinavyopata views nyingi zaidi, ndivyo zawadi yako ya pesa inavyokuwa kubwa.

Tier Views za Jumla (wiki 6) Zawadi ya Pesa
1 5,000 – 9,999 views TZS 100,000
2 10,000 – 19,999 views TZS 150,000
3 20,000 – 34,999 views TZS 200,000
4 35,000 – 49,999 views TZS 250,000
5 50,000 – 74,999 views TZS 300,000
6 75,000 – 99,999 views TZS 350,000
7 100,000 – 124,999 views TZS 400,000
8 125,000 – 149,999 views TZS 450,000
9 150,000+ views TZS 500,000

Kila mshiriki anaweza kushinda mara moja tu. Hairuhusiwi kubadili zawadi za vitu kuwa pesa taslimu. Maelezo kamili katika Sheria na Masharti.

Hisense TV - Zawadi ya Kila Wiki

Zawadi za Kila Wiki

Washindi 3 kila wiki

Zawadi za Kila Wiki

Shinda Kila Wiki

Nafasi ya 1
Hisense TV — mshindi 1 kwa wiki (jumla 5)
Nafasi ya 2
King'amuzi cha DSTV + Kufurushi cha miezi 3 — mshindi 1 kwa wiki (jumla 5)
Nafasi ya 3
Vocha ya manunuzi ya TZS 200,000 — mshindi 1 kwa wiki (jumla 5)

Jedwali la Kila Wiki

Matokeo ya mwisho kwa kila wiki.

Wiki 4: Jumamosi Jul 11 -- Ijumaa Jul 17

Matokeo Yanakuja Hivi Karibuni

Jedwali la Washindi

Huhitaji kuwa mtengenezaji bora ili kupata zawadi. Kusanya views katika wiki sita, fikia kiwango na pata zawadi za pesa. Fuatilia maendeleo yako hapa chini (kumbuka utaona video zilizoidhinishwa tu hapa).

Huoni video yako kwenye jedwali bado? Tunapitia maudhui kila siku (Jumatatu-Ijumaa) na inaweza kuchukua hadi siku 3 za kazi kuonekana. Subiri -- au kama kuna tatizo:
Tuambie

Hujui utengeneze nini?

Tuonyeshe nyakati zinazofanya mpira kuwa wa kipekee. Kwa mfano:

Sherehe za Ushindi

Unasherehekea vipi ushindi wako? Dansi, nyimbo, kufurahia na washikaji

Mila za Siku ya Mechi

Mila za kabla au baada ya mechi mf. Jezi pendwa, chakula, kijiwe chako na washikaji n.k.

Wakati wa Coca-Cola

Fungua Coca-Cola baridi, shiriki na marafiki muda wa mechi

Unapofurahia Goli

Kelele, furaha, kushindwa kuamini

Utani wa Mpira

Uchokozi kati ya mashabiki, utabiri, "nilikuambia"

Huzuni na Drama

Penalti, kadi nyekundu, wakati wa karibu kufunga

Tunachotafuta

Kumbuka haya unapotengeneza video zako.

Muundo

Video ya wima (Reel) iliyochapishwa kwenye Instagram na/au TikTok. Sekunde 30-60 ni bora.

Hashtagi

#NiWakatiwaCocaCola, #NiMsimuwaFifaWorldCup. Tagi @coca_cola_tanzania.

Ubora

Tunataka kuona hisia za kweli za mashabiki – magoli, karibu kufunga, huzuni, furaha, tamaduni, na jadi, n.k.

Onyesha Coke

Video yako lazima ionyeshe mtu akinywa Coca-Cola kutoka kwenye chupa au mkebe kama sehemu ya sherehe za msimu huu wa Kombe la Dunia la FIFA 2026.

Fanya

Do Onyesha Coca-Cola mwanzoni mwa video yako – ikiwezekana sekunde 3 za mwanzo
Do Ifanye iwe sehemu ya msimu wa Kombe la Dunia la FIFA 2026 – hisia za mechi na marafiki
Do Onyesha uhalisia – Hisia za kweli, furaha, huzuni, utani, tamaduni za mpira n.k.
Do Hakikisha una ruhusa ya kurekodi muonekano wa mtu; tumia miziki isio na hakimiliki au pakua nyimbo yetu hapo chini

Usifanye

Don't Usirekodi mechi katika video yako, shindano hili ni kuhusu hisia za mashabiki siyo mechi, tuonyeshe hisia zako kama shabiki
Don't Usionyeshe tabia hatari au unywaji soda kupita kiasi
Don't Usionyeshe watoto chini ya umri wa miaka 13
Don't Usionyeshe maudhui ya utata au ya kukera
Don't Usitumie video zilizozalishwa au kuhaririwa na AI – video yako iwe halisi
Angalia Masharti Kamili ya Maudhui

Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara

Hisi Yote Challenge ni nini?
Shindano la kusherehekea Kombe la Dunia la FIFA 2026. Tengeneza video fupi inayoonyesha hisia zako za kweli unapotazama mpira. Post kwenye page yako, tumia hashtag zinazohitajika, na ujipe nafasi ya kushinda zawadi.
Nani anaweza kushiriki?
Mtu yeyote mwenye umri wa miaka 18 au zaidi nchini Tanzania mwenye akaunti ya umma ya TikTok na/au Instagram. Lazima ujiandikishe kwenye ukurasa huu kabla video zako hazijahesabiwa.
Ninajiandikishaje?
Jaza fomu ya usajili kwenye ukurasa huu na taarifa zako na utapokea barua pepe ya uthibitisho ukishajiandikisha.
Naweza kutumia sauti zinazovuma au mfumo wa meme?
Ndiyo! Sauti zinazovuma, templeti, na mfumo wa meme unahimizwa mradi maudhui ni ya asili na yanafuata miongozo ya changamoto.
Washindi wanachaguliwaje?
Shindano litaendeshwa kila wiki kuanzia Jumamosi saa Sita Usiku (12:00 AM) hadi Ijumaa saa Tano na Dakika 59 usiku (11:59 PM) muda wa Afrika Mashariki. Washindi wa 3 bora wenye views nyingi zaidi kwa wiki hiyo watapata: Nafasi ya 1 – Hisense TV, Nafasi ya 2 – King'amuzi cha DSTV, Nafasi ya 3 – Vocha ya manunuzi yenye thamani ya TZS 200,000. Mwishoni mwa shindano, washiriki watapata nafasi ya kujishindia zawadi za pesa taslimu kulingana na views za video zao.
Video zangu zitaonekana lini kwenye jedwali?
Tunapitia maudhui kila siku (Jumatatu-Ijumaa). Inaweza kuchukua hadi siku 3 za kazi kwa video yako kupitishwa na kuonekana kwenye jedwali. Video hazionyeshwi mara moja.
Naweza kuchapisha kwenye majukwaa mengi?
Ndiyo. Unaweza kuchapisha kwenye TikTok na Instagram. Views kutoka majukwaa yote mawili zinachanganywa kwa jumla yako ya wiki lakini profaili moja tu kwa kila jukwaa itahesabiwa.
Zawadi ni zipi?
Kuna aina mbili ya Zawadi. Zawadi za kila wiki ambapo washiriki watatu bora kwa kila wiki kwa kipindi chote cha shindano watajishindia TV aina ya Hisense, King'amuzi cha DSTV au Vocha ya manunuzi yenye thamani ya laki mbili (TZS 200,000). Aina ya pili ya zawadi ni pesa taslimu zitakazotolewa mwishoni mwa shindano kulingana na jumla ya views ulizopata kutokana na video ulizopost. Angalia sehemu ya Viwango vya Zawadi kwa maelezo kamili.
Views zangu zinaendelea kutoka wiki hadi wiki?
Kuna aina mbili za zawadi. Video ndani ya kipindi cha wiki sita zinahesabiwa kwa zawadi za pesa mwishoni mwa changamoto. Kila wiki pia ni mzunguko mpya wa zawadi za vitu. Ni video zilizochapishwa ndani ya kipindi cha wiki hiyo pekee (Jumamosi hadi Ijumaa) zinazohesabiwa kwa zawadi za wiki hiyo.
Nitaarifiwa vipi nikishinda?
Tutawasiliana na washindi kupitia barua pepe au nambari ya simu waliyotumia kujiandikisha ndani ya siku 7 baada ya matokeo kuthibitishwa. Washindi wataonekana pia kwenye ukurasa wetu wa washindi wa kila wiki.
Nifanye nini kama video yangu imekataliwa?
Utapokea barua pepe inayoeleza kwa nini video yako imekataliwa. Unaweza kurekebisha tatizo na ku-post video yako tena. Hakikisha umesoma Vigezo na Masharti kabla ya kuchapisha ili kuhakikisha video yako inakidhi vigezo.
Naweza kusoma wapi Vigezo na Masharti Kamili?
Pakua au soma vigezo na masharti HAPA.
Coca-Cola

Viungo vya Haraka

Jinsi ya Kushiriki

Jiandikishe

Zawadi

Jedwali la Washindi

Washindi wa Awali

Msukumo

Miongozo

FAQs

Kisheria

Sheria na Masharti

Taarifa za Faragha za Coca-Cola

Mawasiliano

tanzania@coca-cola-football.com

Powered by EnTribe
Privacy Policy Terms of Use